November 18, 2024

newsline

Timely – Precise – Factual

Susan Kihika Ampa Jeff Koinange Ujumbe Ampeleke Uhuru

506 Views

Seneta wa Nakuru Susan Kihika amemkashifu Rais Uhuru Kenyatta kwa madai yake kuwa kulikuwa na njama ya kumshtaki baada ya uchaguzi wa 2017.

Akiongea na Jeff Koinange wa runinga ya Citizen mnamo Jumatano, Machi 30, Seneta wa Nakuru alipuuzilia mbali madai hayo, akibainisha kuwa Rais anafaa kuwaomba Wakenya msamaha kwa kile alichokitaja kuwa propaganda za bei nafuu.

Mbunge huyo alidokeza kuwa madai hayo yamepingwa na Naibu Rais William Ruto na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga, hivyo basi kuthibitisha kuwa Rais alikuwa na nia ya madai hayo.

Mwanahabari mashuhuri Jeff Koinange akiwa katika studio za Citizen TV

Susan Kihika Sanitized by Raila Odinga | Sunset Kenya

Kihika alimtaka Jeff kumwambia Rais Kenyatta kwamba Wakenya wanastahili kujua maelezo yaliyounga mkono madai yake.

“Rais alikuwa anadanganya, anahitaji kuomba msamaha kwa Wakenya. Hata hivyo, kwa vile nimekuambia kuwa DP Ruto na Raila Odinga walijitokeza na kusema, hakuna kitu kama hicho.”

“Hata wabunge walikuwa hawajasikia kitu kama hicho. Kisha unahitaji kumwita Uhuru Kenyatta hapa na ajibu swali hilo ili aweze kutupa maelezo zaidi ndiyo maana naita hii kama propaganda.” Kihika alisema.

Aidha, seneta huyo alichukua muda kuzungumza na Rais moja kwa moja kupitia kamera kuhusu madai ya kuondolewa madarakani.

Sen. Susan Kihika (@susankihika) / Twitter

“Kila kitu ambacho Rais Uhuru amefanya kufikia hapa kujaribu kuhakikisha kwamba anakomesha kasi ya Ruto kimefeli na ndiyo maana ameibuka na madai haya ya kushtakiwa, ambayo ni uongo.”

“Unaweza kunionyesha kamera ambayo ninahitaji kuangalia ili kumhutubia Rais; kwa kweli ni bahati mbaya sana na anahitaji kujitokeza na kutoa ukweli, vinginevyo ajiondoe na aache kuchochea makundi ya kikabila,” alisisitiza.

Seneta wa Homa Bay, Moses Kajwang’ hata hivyo, alidokeza kuwa Rais Kenyatta alikuwa na haki kama raia wa nchi kutangaza maoni na hofu yake.

“Rais ana haki yake kama raia kujieleza na hofu yake,” alisema.

Wakati wa mkutano na wazee wa Mlima Kenya mnamo Jumamosi, Machi 26, inaripotiwa kwamba Uhuru alitangaza hadharani njama za Ruto za kutaka ang’olewe.

Gloves off as Millie Odhiambo and Susan Kihika talk tribal politics on  national TV | Pulselive Kenya

Raila na Ruto wamejitokeza kukanusha madai hayo.

Zaidi ya hayo, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee na Msimamizi wa hafla ya Ikulu alikanusha mazungumzo ya kumuondoa madarakani wakati wa kikao hicho.

“Mimi ndiye niliyekuwa mshereheshaji katika hafla hiyo tangu mwanzo hadi mwisho na ninataka kutangaza leo kwamba hakuna kitu kama hicho kilichotajwa wakati wa mkutano, achilia mbali na rais,” mmoja wa wazee alisema.